Oct 01, 2022 12:09 UTC
  • Kiwango cha vijana kujitoa uhai nchini Marekani chaongezeka

Idadi ya wananchi wa Marekani hususan vijana wanaojitoa uhai imeongezeka kwa kiwango cha kutisha.

Takwimu mpya zilizotolewa Ijumaa na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini humo (CDC) zinaonesha kuwa, idadi ya Wamarekani wanaojiua iliongezeka kutoka 46,000 mwaka 2020, hadi 47,650 mwaka jana.

Ongezeko hilo la mwaka jana linaashiria mwisho wa miaka miwili ya kunakiliwa kiwango kidogo cha Wamarekani kutojitoa uhai. CDC inasema kuwa, aghalabu ya kesi za kujitoa uhai zilizoshuhudiwa mwaka jana ni miongoni mwa vijana wa kiume waliokuwa na umri kati ya miaka 15 na 24.

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani kimesema kuwa, kujitoa uhai ndiyo sababu kuu ya pili ya vifo miongoni mwa vijana wenye miaka baina ya 10-34 nchini humo.

Msongo wa mawazo

Mwenendo huo wa kujitoa uhai haushuhudiwi tu miongoni mwa raia wa Marekani, lakini pia miongoni mwa maafisa usalama wa nchi hiyo. Ripoti ya karibuni ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inaonesha kuwa, zaidi ya maveterani elfu 45 wa jeshi la Marekani au watu waliohudumu katika jeshi katika kipindi cha miaka sita iliyopita wamejiua.

Inaarifiwa kuwa, kwa wastani, wanajeshi 20 wa Marekani hujitoa uhai kila siku, suala linaloonesha kuwa idadi ya wanajeshi wanaopoteza maisha yao kwa kujiua ni kubwa zaidi kuliko wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita vya Iraq na Afghanistan.

Tags