Oct 02, 2022 12:07 UTC
  • Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
    Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz

Chama cha mrengo wa kushoto cha Ujerumani kimekosoa vikali hatua ya serikali mpya ya muungano ya nchi hiyo ya kutoa leseni ya kuuza silaha kwa serikali ya Saudi Arabia.

Janine Whistler, mkuu wa Chama cha Kushoto cha Ujerumani, ametangaza kwamba idhini ya serikali mpya ya muungano ya Ujerumani ya mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia ni kitendo kichafu, cha kutowajibika na kashfa.

Sevim Dağdelen, mtaalamu wa mambo ya nje wa chama cha mrengo wa kushoto cha Ujerumani na mkuu wa Kamati ya Mahusiano ya Nje ya chama hicho katika Bunge Kuu la nchi hiyo "Bundestag", amekosoa vikali utoaji wa leseni ya kuuza silaha kwa Saudi Arabia na kukitaja kitendo hicho kuwa ni uhalifu.

Ni baada ya serikali mpya ya muungano ya Ujerumani kuanza tena usafirishaji wa siri wa silaha kwa Saudi Arabia.

Vyombo vya habari vya Ujerumani, vikiwemo Spiegel na shirika la habari la DPA, vimetangaza kuwa serikali mpya ya nchi hiyo imeidhinisha kandarasi mpya za kusafirisha tena silaha kwa Saudi Arabia.

Haya yanajiri licha ya kuwa hapo awali Berlin ilipiga marufuku uuzaji wa silaha kwa Riyadh kutokana na mashambulizi ya Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen na mauaji ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari mkosoaji wa Saudia.

Silaha za nchi za Magharibi zinatumiwa na Saudia kuua raia wa Yemen

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani, ripoti kuhusu uamuzi wa Berlin wa kuiuzia tena silaha Saudi Arabia zilifichuliwa baada ya Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz kuzitembelea nchi za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar.

Saudi Arabia inatumia silaha za nchi za Magharibi kuua watoto, wanawake na raia wasio na hatia ya Yemen na hadi sasa maelfu wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi ndani na nchi ya nchi hiyo. 

Tags