Oct 03, 2022 08:12 UTC
  • Hillary Clinton
    Hillary Clinton

Uwezekano wa Hillary Clinton kugombea kwa mara ya tatu katika uchaguzi wa urais wa Marekani umeongezeka zaidi.

Hillary Clinton, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani aliyekuwa mpinzani wa Kidemokrati wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, katika uchaguzi wa 2016, awali alisema katika mahojiano na Financial Times kwamba Marekani iko kwenye ukingo wa kupoteza demokrasia, na suala hilo litakuwa la kuogofya zaidi katika uchaguzi wa urais wa 2024 kwa kutilia maanani wagombea waliopo sasa.

Msaidizi wa zamani wa Bill Clinton, Dick Morris, alisema katika mahojiano ya redio kuhusu uwezekano wa Hillary Clinton kugombea tena kwamba: Anajiandaa kuingia katika uchaguzi wa 2024 kama chaguo la wastani kwa Wanademokrasia.

Akiashiria kauli za hivi karibuni za Hillary Clinton kwamba Wamarekani hawaamini mipaka iliyo wazi, Morris amesema, "Kila siku kunajitokeza dalili zaidi za uamuzi wa Hillary kushiriki katika uchaguzi ujao wa urais kama mgombea wa wastani."

Msaidizi huyo wa zamani wa Bill Clinton amesema kuna uwezekano wa chama cha Democrats kumpendelea Hillary Clinton kuliko Rais wa sasa wa Marekani, Joe Biden, kwa sababu ya hofu ya kushindwa, na kuongeza kuwa: Wademokrati wanaona kuwa, uwezekano wa kushinda mgombea mwenye misimamo ya wastani ni mkubwa zaidi katika uchaguzi ujao.

Clinton

Itakumbukwa kuwa, Hillary Clinton, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani wakati wa utawala wa Barack Obama, alizomewa kama mhalifu wa kivita alipoingia Chuo Kikuu cha Queen katika mji mkuu wa Ireland Kaskazini.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani pia amekiri katika kitabu chake cha "Machaguo Magumu" (Hard Choices) kwamba kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) liliundwa na Marekani.