Oct 04, 2022 02:14 UTC
  • Lavrov: Marekani inaisambaratisha Ukraine kwa ajili ya kuishinikiza Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, Marekani inasababisha kupata hasara kubwa na kusambaratishwa Ukraine kwa ajili ya kutoa vitisho kwa Russia.

Sergey Lavrov alisema hayo jana mbele ya Bunge la Russia (DUMA) na huku akigusia jinsi Marekani inavyoitumia vibaya Ukraine kwa ajili ya kutoa vitisho kwa Russia amesema, Moscow inafanya tofauti na Washington. Amesema, Marekani inatumia nchi nyingine ya mbali kutoa vitisho kwa mataifa ya dunia, wakati Russia inachofanya ni kujibu vitisho tu vilivyoko kwenye mipaka ya ardhi yake.

Matamshi hayo ya Lavrov yamekuja baada ya mikoa minne ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporozhye ya Ukraine kupiga kura ya maoni na kujiunga rasmi na ardhi mama ya Russia. 

Majimbo manne mapya ya Ukraine yaliyopiga kura na kujiunga na ardhi ya Russia.

 

Amesema, mchakato uliotumika ya kuyaunganisha majimbo hayo manne na ardhi ya Russia ni wa kimantiki kabisa. Demokrasia imefuatwa. Wananchi wenyewe wa majimbo hayo wameshiriki kwenye kura ya maoni na asilimia kubwa wameamua kujitenga na Ukraine na kujiunga na Russia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kuwa, wananchi wa maeneo hayo walishindwa kuvumilia kuwa chini ya serikali ya Ukraine kutokana na serikali hiyo ya Kyiv kufanya jinai kubwa na mashambulio ya mara kwa mara dhidi yao.

Jana Jumatatu, Bunge la Russia (DUMA) lilipasisha hati ya kujiunga na Russia, majimbo hayo manne ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporozhye.

Tags