Oct 04, 2022 07:38 UTC
  • Shirika la IMF limejitosa kwenye vita vya Ukraine?

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) unatafakari suala la kuipa Ukraine dola bilioni 1.3 kama fedha za dharura.

Bodi Kuu ya Shirika hilo la Fedha Duniani la Umoja wa Mataifa inatazamiwa kufanya kikao siku ya Ijumaa, kutathmini ombi la Ukraine la kupewa fedha hizo.

Vyanzo viwili vilivyo karibu na kadhia hiyo vimenukuliwa na shirika la habari la Reuters vikisema kuwa, maafisa wa IMF wameandaa nyaraka zinaonesha kuwa Ukraine imepasi vigezo vinavyostahili kwa ajili ya kupewa fedha hizo.

Ingawaje Ukraine inadai kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili kushughulikia uhaba wa chakula, lakini baadhi ya wadadisi wa mambo wanatilia shaka suala hili. Machi mwaka huu, IMF iliipa Ukraine 'msaada wa dharura' wa dola bilioni 1.4, muda mfupi baada ya kuanza vita nchini humo.

Vita Ukraine

Haya yanajiri wiki mbili baada ya Ursula Van der Leyen, Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya kwenda Kiev, mji mkuu wa Ukraine katika ziara yake ya tatu nchini humo tangu kuanza mashambulizi ya Russia dhidi ya nchi hiyo.

Vita kati ya Russia na Ukraine vilianza Februari 24. Nchi za Ulaya na Marekani zimechochea na kukoleza moto wa vita na mapigano nchini humo kwa kuzidisha mashinikizo ya vikwazo dhidi ya Russia na kuipatia Kiev kila aina ya silaha nyepesi na nzito

Tags