Jul 25, 2021 01:18 UTC
  • Jumapili, 25 Julai, 2021

Leo ni Jumapili tarehe 14 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1442 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 25 Julai 2021 Miladi.

Siku kama ya leo miaka 127 iliyopita, vita kati ya Uchina na Japan vilianza kwa mashambulio yaliyofanywa na vikosi vya jeshi la Japan dhidi ya maeneo ya pwani ya Uchina. Vita hivyo vilitokea baada ya mashambulio yaliyofanywa na Japan kwa lengo la kuiteka ardhi kubwa ya Peninsula ya Korea na kaskazini mwa China. Japan ndiyo iliyoshinda katika vita hivyo kutokana na kujizatiti vyema kwa silaha za kisasa. ***

Bendera za Jpana na China

 

Katika siku kama ya leo miaka 83 iliyopita, Wapalestina 62 wasio na hatia  waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea kwa nyakati tofauti katika soko la kuuzia mboga za majani huko Palestina. Makundi ya kigaidi ya Wazayuni ndiyo yaliyotega mabomu hayo mawili na lengo lao lilikuwa ni kuzusha hali ya machafuko na ukosefu wa amani kwa Wapalestina. ***

 

Miaka 82 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Ayatullah Fayyaz Zanjani fakihi na msomi mahiri wa elimu ya Usuul. Awali alisoma masomo yake kwa Mujtahidi Akhund Mullah Muhammad. Baadaye akahudhuria masomo kwa walimu mahiri wa zama hizo mjini Tehran kama Mirza Muhammad Hassan Ashtiyani na kuwa mahiri katika taaluma za fikihi, Usuul, mantiki na tafsiri. Mwanazuoni huyo alikuwa Marjaa Taqlidi wa Zanjani. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 alikuwa mmoja wa waeneza mafundisho ya Ahlul Bayt na waalimu wakubwa wa Maktaba ya Ushia. ***

Ayatullah Fayyaz Zanjani

 

Na siku kama ya leo miaka 28 iliyopita, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena lilianzisha mashambulizi makubwa ya anga na baharini huko kusini mwa Lebanon. Mashambulizi hayo yalikuwa operesheni kali zaidi ya kijeshi kuwahi kufanywa na Wazayuni dhidi ya Lebanon baada ya mashambulio waliyoyafanya dhidi ya ardhi nzima ya Lebanon mwaka 1982. ***

Mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa Lebanon

 

Tags