-
Waziri Mkuu wa zamani wa Kuwait azuiwa kusafiri nje ya nchi kwa tuhuma za ufisadi
Mar 30, 2021 08:02Mahakama ya Mawaziri inchini Kuwait imempiga marufuku kusafiri nje ya nchi Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo. Jaber al Mubarak al Hamad all Sabah anakabiliwa na kesi ya ufisadi wa mamia ya mamilioni ya dinari za mfuko wa hazina wa jeshi la nchi hiyo.
-
Spika wa Bunge la Kuwait: Nchi yetu inapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Israel
Jan 20, 2021 07:51Spika wa Bunge la Kuwait amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, msimamo wa nchi yake kuhusiana na Palestina uko thabiti na si wenye kubadilika na kwamba, nchi hiyo inapinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani yaafiki kuziuzia silaha Misri, Kuwait na Saudia
Dec 30, 2020 06:17Katika mwendelezo wa siasa za White House zinazolenga kuuza silaha zaidi; Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza kuwa imeafiki kutekelezwa mikataba ya kuziuzia silaha Misri, Kuwait na Saudi Arabia.
-
Kuwait: Jukumu la usalama wa Ghuba ya Uajemi ni la nchi zote za eneo hilo
Dec 15, 2020 11:34Waziri Mkuu wa Kuwait amesema kuwa, suala la kulinda usalama wa Ghuba ya Uajemi ni jukumu la nchi zote za eneo hilo na hakuna nchi yoyote inayoweza kujivua na jukumu hilo.
-
Emir wa Kuwait akubali hatua ya serikali kujiuzulu
Dec 07, 2020 01:17Emir wa Kuwait Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ameafiki hatua ya kujiuzulu serikali ya nchi hiyo. Kujiuzulu serikali nchini Kuwait ni jambo la kawaida ambalo hufanyika baada ya uchaguzi. Siku ya Jumamosi uchaguzi wa bunge ulifanyika nchini Kuwait.
-
Iran yatuma salamu za rambi rambi baada ya kuaga dunia Amir wa Kuwait
Sep 30, 2020 08:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Sheikh Swabah al-Ahmad Jabir as-Swabah, Amir wa Kuwait.
-
Amir wa Kuwait, Sheikh Sabah (91) aaga dunia nchini Marekani
Sep 30, 2020 04:39Amir wa Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 91.
-
Mirengo ya siasa Kuwait yakanusha kujiunga na mkumbo wa kutangaza uhusiano na Wazayuni
Sep 20, 2020 11:21Mirengo mbalimbali ya kisiasa ya Kuwait imekanusha madai ya rais wa Marekani, Donald Trump aliyedai kuwa nchi hiyo nayo itajiunga karibuni hivi katika mkumbo wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.
-
Msafara wa silaha na zana za kijeshi za Marekani kutoka Kuwait waingia Basra, Iraq
Aug 17, 2020 13:14Duru moja ya masuala ya usalama ya Iraq imeripoti kuwa, msafara wa malori ya kijeshi ya Marekani yaliyosheheni silaha na zana nyingi za kijeshi umeingia katika ardhi ya nchi hiyo kwa lengo la kuhamishia silaha na zana hizo katika kituo cha kijeshi cha Ainul-Asad.
-
Spika wa Bunge la Kuwait ataka nchi za Kiarabu zikabiliane na Israel
Jul 05, 2020 03:46Spika wa Bunge la Kuwait ametaka nchi za Kiarabu zichukue hatua kali za kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuteka maeneo zaidi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.