-
Mali yakataa wito wa UN kuhusu madai ya ukiukaji haki za binadamu
Jul 01, 2022 08:02Serikali ya Mali imesema haitaufanyia kazi wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuitaka iruhusu wanajeshi wa kulinda amani wasafiri ndani ya nchi hiyo kwa uhuru ili kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
-
UNODC: Mamilioni ya vijana duniani wamezama katika uraibu wa mihadarati
Jun 28, 2022 07:57Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayohusika na Jinai na Mihadarati (UNODC) imesema watu zaidi ya milioni 284 duniani wenye umri kati ya miaka 15 na 24, walitumia aina mbalimbali ya mihadarati mwaka juzi 2020, hilo likiwa ni ongezeko la asilimia 26 katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
-
Bachelet ataka uchunguzi huru wa mauaji ya halaiki nchini Ethiopia
Jun 24, 2022 14:26Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa sambamba na kulaani mauaji ya halaiki ya hivi karibuni ya raia hususan wanawake na watoto wadogo magharibi mwa Ethiopia, ameitaka serikali ya Addis Ababa kufanya uchunguzi huru, wa kina, wa haraka na usioegemea upande wowote.
-
UN: Mwanahabari Shireen Abu Akleh aliuawa na wanajeshi wa Israel
Jun 24, 2022 13:26Umoja wa Mataifa umesema taarifa ulizokusanya zinaonesha kuwa, Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa televisheni ya al-Jazeera ya Qatar aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya Israel.
-
UN: Usipopatikana msaada wa haraka hali ya kibinadamu itakuwa mbaya zaidi Nigeria
Jun 22, 2022 07:57Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria ambaye pia ni mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini humo Matthias Schmale amesema zaidi ya watu milioni 4.1 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula katika msimu wa mwambo utakao anza hivi karibuni.
-
Mshauri wa Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kukomeshwa mizozo nchini Libya
Jun 21, 2022 02:41Stephanie Williams, Mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya, ametoa wito kwa uongozi wa Baraza la Serikali ya Libya kukutana ndani ya siku 10 ili kutafuta suluhisho la masuala yenye utata yanayozua hitilafu baina ya makundi mbalimbali.
-
UN: Zaidi ya watu milioni 7 wamekuwa wakimbizi nje ya Ukraine mbali na wakimbizi wa ndani
Jun 20, 2022 11:52Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, vita vya Ukraine ni moja ya sababu za ongezeko la wakimbizi ulimwenguni na kwamba hadi hivi sasa mamilioni ya watu wameshakuwa wakimbizi kutokana na vita hivyo.
-
UN yajitenga na mpango wa kuwahamishia wakimbizi wa UK nchini Rwanda
Jun 11, 2022 10:20Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limejiweka mbali na madai kuwa linaunga mkono mpango wa kuwahamishia Rwanda wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza.
-
UN: Israel kupora ardhi na kuwabagua Wapalestina, chachu ya ghasia na migogoro
Jun 08, 2022 10:53Timu ya ngazi ya juu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema hatua ya utawala haramu wa Israel ya kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina na kuwafanyia Wapalestina vitendo vya kibaguzi ndio sababu kuu ya kushuhudiwa mawimbi ya ghasia zisizokwisha katika ardhi hizo zilizoghusubiwa.
-
Katibu Mkuu wa UN: Tuna dunia moja pekee, tunapaswa kuilinda
Jun 05, 2022 08:16Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema, sayari dunia ndio makazi pekee ya watu, akimaanisha kuwa hakutakuwa na pa kukimbilia ikiwa itachafuliwa na kusisitiza kwamba “ni muhimu kulinda afya ya anga yake, utajiri, na aina mbalimbali ya viumbe vilivyoko duniani bila kusahau ikolojia yake na rasilimali lukuki.”